Ziara ya kwanza ya manesi toka Bugando Medical Center kwenda Missionary Clinic kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.
Octoba 2013, manesi wanne (wakike wawili na wakiume wawili) toka Mwanza walipata fursa ya kujiendeleza kwa vitendo huko Würzburg katika Missionary Clinic, kwa muda wa wiki tatu.
M.W.A.N.Z.A. e.V. iliandaa muda wa mapunziko hili waweze kujionea wenyewe mji rafiki wa Mwanza. Waliweza kukaribishwa na Mayor Marion Schäfer-Blake katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Würzburg.