Selected Articles in Swahili languageRipoti zilizochaguliwa  kwa Kiswahili Yaliyomo ya kurasa hizi hayajamalizika bado. Tafadhali urudi hapo baadaye.

ZOOM – Uzoefu wa ubaguzi wa rangi na ukoloni katika mahusiano ya miji / mapacha

Mnamo Machi 22 saa 19 p.m. kutakuwa na mazungumzo ya Zoom na waigizaji
Mwanza, Würzburg’s twin city.
“Uzoefu wa ubaguzi wa rangi na ukoloni katika mahusiano ya miji / mapacha”
Watu kutoka miji yote miwili wanaripoti hii.
Tuliwauliza watu kutoka Mwanza kama kuna ubaguzi wa rangi au ukoloni katika nchi yao:

  • Dk. George Mutalemwa, kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania (SAUT)
  • Joseph Senais, mwanafunzi wa udaktari kutoka Tanzania (Chuo Kikuu cha Cottbus, Mafunzo ya Urithi wa Dunia)
  • Boniventura Toto, mkurugenzi wa kituo cha walemavu,
  • Sr. Denise Mattle, mtawa wa Kifransisko ambaye alitumia maisha yake yote nchini Tanzania,
  • Deo Mrisho, mwanafunzi wa Kitanzania ambaye kwa sasa anasoma Schweinfurt,

Pia watu ambao wanahusiana na kuunganishwa kwa jiji haa:

  • Dominik Wershofen kutoka ofisi ya mapacha ya jiji,
  • ikiwezekana Helmut Stahl na Anunsiata, walioa hapa,
  • Thomas Barcatta, kutoka kwa Afisa Uhusiano aliyejitolea wa IT wa MWANZA eV

— na bila shaka ninyi nyote pia.

Tunatazamia kubadilishana.

Jiunge na Mkutano wa Zoom
https://us06web.zoom.us/j/87506171674?pwd=XAQraiWMFfZeUfNiA8Bxa9HCF4lomo.1
Kitambulisho cha Mkutano: 875 0617 1674; Nambari ya kitambulisho: 776815

Watu Wenye Albino Tanzania

Zoom-Meeting:
https://us06web.zoom.us/j/84645588645?pwd=Q3BWVGg5VE1tMzFzL1pySWFiU1puQT09 https://us06web.zoom.us/j/84645588645?pwd=Q3BWVGg5VE1tMzFzL1pySWFiU1puQT09
Meeting-ID: 846 4558 8645
Kenncode: 736161

Basi la watoto walemavu kwa shule ya chekechea

Mnamo mwaka wa 2022, tulifanikiwa kuandaa mchango wa ‘dalla dalla’ ya Huruma. Nusu ya mchango imepeanwa na PartnerKaffe e.V., waliochanga 6.000,00 € – zilizoombwa na MWANZA eV. Pesa kiasi hicho zimeongezwa na shirika la Mwanza Sports Charity kwa basi ndogo lililotumika. Sasa usafiri wa wanafunzi 40 au zaidi kutembelea shule umehakikishwa. Hata hivyo, ni tone ndogo la ukali kwamba, kwa sasa itabidi wazazi walipe usafiri.

Lori la taka kabla ya kusafirishwa

Novemba 2013 M.W.A.N.Z.A. e.V. ilitoa lori la taka kwa ajili ya kusaidia usafi wa jiji la Mwanza. Lori hilo lilikuwa ni la tatu kulotewa kwa ajili ya usafi wa jiji la Mwanza, katika kipindi cha miaka 20 ya urafiki wa majiji haya mawili.

Lori lilisheheni zawadi mbali mbali, kama mavazi ya kuwakinga watu wa zimamoto, viatu kwa ajili ya watoto yatima, vifaa vya wasioona, samani mbali mbali kutoka shule za awali ya Montessori.

Lori lilifanyiwa ukaguzi uliokidhi viwango vya TÜV (car controlling) ili liweze kusaidia mji rafiki la Mwanza. Mwaka uliopita Lori hili lilikaguliwa na Tito Mahinya kutoka halmashauri ya jiji la Mwanza.

Gharama za kusafirisha lori hili hadi bandari ya Daressalam ziligharamiwa na M.W.A.N.Z.A. e.V. na wizara ya ushirikiano wa uchumi na maendeleo (BMZ, GTZ) Baada ya kufika Daressalaam serekali ya Tanzania itahusika na gharama za kutoa gari bandarini na kulisafirisha hadi Mwanza umbali wa km zisizopungua 1000.

Ziara ya kwanza ya manesi toka Bugando Medical Center kwenda Missionary Clinic kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.

Octoba 2013, manesi wanne (wakike wawili na wakiume wawili) toka Mwanza walipata fursa ya kujiendeleza kwa vitendo huko Würzburg katika Missionary Clinic, kwa muda wa wiki tatu.

M.W.A.N.Z.A. e.V. iliandaa muda wa mapunziko hili waweze kujionea wenyewe mji rafiki wa Mwanza. Waliweza kukaribishwa na Mayor Marion Schäfer-Blake katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Würzburg.

JIJI RAFIKI NA MWANZA LAKABIDHI MRADI KWA WAVUVI WA DAGAA ZIWA VICTORIA

Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (katikati) akibonyeza swichi ya taa za kuchaji zinazotumia umeme wa solar kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi wa uvuvi wa karabai zinazotumia nishati ya jua, kushoto kwake ni rais wa Umoja wa majiji rafiki (jiji la Wuerzburg na jiji la Mwanza) Michael Stolz’ toka nchini Ujerumani na kulia kwake ni mjumbe aliyeambatana na rais huyo, pembeni kabisa ni kiongozi wa BMU Luchelele iliyopo kata ya Mkolani ambao utakuwa ni wa majaribio kabla ya kuenea maeneo mengine kanda ya ziwa Victoria.

source www.gsengo.blogspot.com:  Saturday, November 10, 2012

Ziara ya timu ya futbol kutoka Mwanza Ujerumani

Wapendaji wa Futbol Ujerumani waliona ajabu timu U20 ya Sports Academy Mwanza ilivyiocheza kwenye mechi mbalaimbali walipozurua Ujerumani.
Futbol Academy iliundwa mwaka wa 2009 yenye mipira miwili na watoto hamsini hivi. Siku hizi imekuwa ni Academy yenye sifa sana kwa wacheza vijana wenye umri wa miaka nana hadi ishirini.
Katika ziara ya vijana hao hadi leo hakuna timu ya federal league ya vijana ambayo ingewashinda. Walishinda Youth champion VfB Stuttgart 3:2. Timu za 1860 Munich, TSC Hoffenheim na Greuther Fürth waliachana mabao sawa.
Vijana hao walijifanya marafiki wengi wakitembelea mashule na kundi za watoto na kufundishana juu ya hali ya maisha.
Mmojawapo wa michezo ya mwisho ulikuwa dhidi ya vijana wa U19 ya 1. FC Nuremberg. Hata timu hii imeshindwa na vijana wa Mwanza 3:1.
Jumatatu tarehe 6 Agosti vijana wa Mwanza walipanda ndege kurudi nyumbani ambapo bila shaka watakuwa na mengi ya kusimulia.

(Zur Bildergalerie!)

Die Fußballüberraschung des Jahres, das U20-Team der TSC Sports Academy Mwanza / Tansania, kehrt zum Abschluss seiner Deutschlandreise nach Würzburg zurück. Mit im Gepäck sind beachtliche Erfolge. Kaum zu glauben, dass diese Jungs vor noch nicht allzu langer Zeit noch reine Straßenfußballer waren!

Im Jahr 2009 auf einer “holprigen Wiese” in Würzburgs Partnerstadt Mwanza mit zwei Bällen und fünfzig Kindern gegründet, hat die gemeinnützige deutsch-tansanische Institution sich durch das ehrenamtliche Engagement zahlreicher Studenten Süddeutschlands zur besten Nachwuchsakademie Tansanias entwickelt. Das Monatsbudget für 130 Jungen und Mädchen im Alter von 8 – 20 Jahren hat im ersten Jahr 200 Euro betragen. 2010/2011 sind es 500 Euro gewesen und im letzten Jahr 1000 Euro. Bis vor fünf Wochen hat man noch eine Schnur zwischen zwei Stangen als Tor genutzt, viele Spieler waren nur mangelhaft ernährt und sie leben weiterhin ohne fließend Wasser und Strom.

Noch keinem A-Jugendbundesligisten ist es gelungen, das TSC-Team zu besiegen. Gegen den deutsche Juniorenrekordmeister VfB Stuttgart hat TSC mit 3:2 gewonnen. Weiter gab es drei hervorragende Unentschieden:2:2 gegen 1860 München, 1:1 gegen die TSC Hoffenheim, sowie 0:0 gegen SpVg. Greuther Fürth.

Die Herzen gewonnen: Wo immer TSC auftritt, schließen sich Spieler und Bevölkerung gegenseitig ins Herz. In Workshops mit Schulen und Kindergruppen vermitteln die Spieler, wie sie in Tansania leben. In ihrer Freizeit lassen sie Kinderherzen höher schlagen und tauschen sich mit Jung und Alt bei verschiedensten Gelegenheiten und Einladungen aus.
Beim U19 Hekatron-Turnier um den Vita-Classica-Pokal in Bad Krotzingen-Hausen am Wochenende ist es nur dem FC Basel gelungen, im Finale die TSC-U20 zu schlagen – und das auch erst im Elfmeterschießen.
Ergebnisse der Gruppenspiele: Stuttgarter Kickers – TSC 1:1, TSC – VfL Bochum 0:0. Halbfinale: SC Freiburg – TSC 1:1, 5:6 nach Elfmeterschießen.

Finale: TSC –  FC Basel 1:1, 6:7 nach Elfmeterschießen.
Am Montag, 30. Juli 2012 zeigten die Nachwuchskicker aus Mwanza, Würzburgs Partnerstadt in Tansania, in vier Würzburger Schulen, wie Kinder und Jugendliche in Tansania leben: Mittelschule Heuchelhof, Dag-Hammarskjöld-Gymnasium, Mönchbergschule und Gymnasium Veitshöchheim. Diese interkulturellen Begegnungen waren eine gute Möglichkeit, in eine fremde Welt mit manchmal auch ähnlichen Problemen abzutauchen. Am Abend gab es eine Trainingseinheit mit den mit Blindenfußballern des BFW Veitshöchheim und mit den Jugendlichen des Grombühler Sportvereins.

Am Mittwoch, 1. August findet ein Benefiz-Turnier zu Gunsten des tansanischen Fußball- und Straßenkinderprojekts “TSC Academy Mwanza” statt. Es spielen neben der TSC U20 (Spieler zwischen 15 und 20 Jahre alt) die U19 Mannschaften vom 1. FC Nürnberg sowie des Würzburger FV auf dem Gelände des SV 09 in der Mainaustraße 36. Kinder zum Einlaufen können unter info@mwanza.de gemeldet werden.
Am Donnerstag, dem 2. August gestaltet TSC einen ganzen Tag bei der Kinderfreizeit auf dem Sanderrasen.

Weitere aktuelle Infos zur Deutschlandreise gibt es auf den Facebook-Seiten der Sports AcademY:

Dort findet sich auch eine Auswahl an Pressestimmen

Redio Deutsche Welle yaripoti

Ziara ya Wanafunzi wa sayansi kimu toka Mwanza katika redio Deutsche Welle

Asumpta Ngonyani akutana na wanafunzi wa Kitanzania wanaotembelea Ujerumani, kuzungumzia umuhimu wa ziara za masomo na mpango wa kubadilishana wanafunzi katika kuwajenga kitaaluma.

Kusoma kuna njia nyingi na moja ya njia hizo ni kutembea na kujifunza mambo kwa njia ya mbadilishano. Ndivyo ziara ya kimasomo ya wanafunzi wa vyuo vya mafunzo ya ujasiriamali vya Tanzania (VETA) inavyothibitisha.
Mtayarishaji/Msimulizi: Asumpta Ngonyani-Lattus
Mhariri: Othman Miraji
Usikilize redio DW hapa

Deutsche Welle Kiswahili sent an interview on the stay of VETA students in Germany (9 minutes). 

Wanafunzi toka Mwanza watembelea Wuerzburg – Mei 2011

Wanafunzi wa Domestic Science toka Mwanza watembelea Wuerzburg – Mei 2011

Wanafunzi wa Wuerzburg Shule ya Domestic Science, wakisaidiwa na mwalimu wao, waliandaa vifaa kama tauli vyenye majina ya wageni wao:

kundi la wanafunzi wakiandaa vifaa kwa ajili ya wageno toka Mwanza

 

Wageni wa Mwanza wakipokelewa Kiwanja cha ndege FrancfortWageni toka Mwanza walipokelewa na kundi toka Wuerzburg kwenye kiwanda cha ndege Frankfort.

Mwalimu Mkuu Doris Mehling (Klara-Oppenheimer-Schule), Mwalimu Homaira Mansury (Frankenwarte Akademy), Michael Stolz (Mwenyekitii wa M.W.A.N.Z.A. e.V.), Asumpta Lattus (Mtanzania, atatafsiri), na wanafunzi wanne wa domestic science waliotembelea Mwanza July 2010.

 

 

 

 

 

 

Kundi la wageni wa Mwanza Senta ya mikutano Frankenwarte

 

 

 

 

 

 

Angalia pia:

Wanafunzi toka Wuerzburg watembelea Mwanza (Mwaka wa 2010)

 

 

 

 

 

 

wageni wakitembelea soko

 

 

 

Mama Eva-Maria Barklind-Schwander akiwaonyesha wageni mji wa Wuerzburg awaongoza kwenda sokoni. Huyu Mama aongoza idara ya Wuerzburg International katika utawala wa mji.

TUNAWEZA – KITUO CHA SHUGHULI NA MSAADA WA AJIRA KWA VIJANA WENYE ULEMAVU

TUNAWEZA –
KITUO CHA SHUGHULI NA MSAADA WA AJIRA KWA VIJANA WENYE ULEMAVU

WALENGWA WETU
Tunawafundisha vijana wa dini na jinsia zote wenye ulemavu waliofikia umri wa miaka 14 na kuendelea. Kipaumbele zaidi ni vijana waliomaliza elimu ya msingi katika vitengo vya elimu maalum vilivyo katika jiji la Mwanza na maeneo ya jirani.

HUDUMA ZETU
• Tunafundisha ujuzi wa maisha na ufundi kwa kipindi cha miaka miwili
• Tunafungua kituo saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni, Jumatatu mpaka Ijumaa
• Tunawasaidia vijana kupata nafasi za kazi kulingana na uwezo na ulemavu wao
• Tunatoa ushauri kwa familia za watoto na vijana wenye ulemavu juu ya upatikanaji wa hudumu mahali tofauti
• Tunatoa semina kwa wazazi/walezi na asasi juu ya kuboresha maisha ya vijana wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na mafunzo ya lugha ya alama

KAZI ZETU ZA KILA SIKU
Vijana hujipatia maarifa ya kazi kupitia miradi tofauti.

BUSTANI
Vijana hushiriki kazi za kuanzisha na kutunza bustani za mbogamboga,
matunda na maua. Pia wanajifunza kutunza mazingira na vifaa na kutengeneza dawa kutokana na mimea ya asili.

UPISHI NA USAFI
Jikoni vijana hupika vyakula vya kiasili na vya kigeni. Wanajifunza usalama wa vyakula na matumizi sahihi ya vifaa vya jikoni.

USHONAJI NA UPIKAJI WA BATIKI
Katika miradi hii vijana wanaelekezwa jinsi ya kutumia cherehani, kutengeza batiki kwa kutumia njia tofauti na kuzalisha bidhaa rahisi ili kujiletea kipato baadaye.

ELIMU YA UJUZI WA MAISHA
Wanafunzi wetu hujifunza juu ya afya, mawasiliano na wanajamii, mambo yanayohusu thamani ya vitu na utu pamoja na utamaduni.
Zaidi ya hayo hufundishwa namna ya kuanzisha na kuendesha biashara ndogo ndogo.

USHIRIKIANO NA WAZAZI
Wazazi hukutana kila baada ya miezi miwili kujadiliana juu ya maendeleo
ya vijana wao kituoni.
Wazazi hushiriki kazi kituoni kulingana na mahitaji ili kujijengea uwezo kwa manufaa ya baadaye ya watoto wao.
Wazazi huchangia gharama kidogo kwa ajili ya chakula.

ASASI YA TUNAWEZA
Ilianzishwa na kusajiliwa mwaka 2009 na watu 12 wenye nia ya kuinua na kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu.

MALENGO YETU
• Kuwapatia vijana wenye ulemavu elimu ya ujuzi wa maisha na ufundi ili waweze
kujitegemea na kujipatia kipato
• Kuwaandaa na kuwawezesha vijana wenye ulemavu kupata na kuendelea na kazi katika soko la ajira au kujiajiri wao wenyewe baada ya kupata ujuzi
• Kuanzisha na kuendesha kituo cha kazi ambacho kinawapatia mazingira bora vijana wenye ulemavu
• Kutetea haki za watu wenye ulemavu