Dagaa, Ugali na Kisamvu – Wanafunzi toka Wuerzburg watembelea Mwanza
Dagaa, Ugali na Kisamvu
Kundi la wanafunzi wa domestic science toka Wuerzburg kwenye ziara ya Mwanza
Hiki kilikuwa chakula cha kwanza ambacho Joyce Kinabo aliwatambulishia wanafunzi tisa toka Shule ya „Klara Oppenheimer“ – Wuerzburg. Kabla ya zoezi hili huyo mwalimu wa domestic science wa Senta ya VETA – Mwanza iliwaingiza wageni wake katika masharti ya kiafya (hygiene) ya Tanzania. Dagaa ni chakula kipendwacho kabisa sehemu za Lake District. Tena ugali – kila Mtanzania ugenini asifu ugali ambao ni chakula chake cha kila siku tangu siku za utoto.
Wanafunzi wawili waliwaonyesha wageni wa Kijerumani jinsi ya kula na mikono. Wajerumani walijali namna hiyo ya kula: „ni tamu zaidi ukila na mkono“.
Watanzania nao walipikiwa Kijerumani, pamoja na maonyesho ya urembo wa meza na huduma mezani. Vyakula vyote vilinunuliwa madukani na sokoni.
Waalimu Joyce Kinabo na Flaviana Minde walikuwa wamepanga ratiba kufuatana na mahitaji ya wageni. Mwalimu Doris Mehling (Wuerzburg) alitambua kwamba „kwa kweli, walijitahidi sana wakipanga ziara hiyo.“ Kufuatana na uzoefu wa Shilika la M.W.A.N.Z.A.
(Wuerzburg) wanafunzi wa Kijerumani waliweza kutembelea taasisi nyingi zaidi, kama vile:
-
Nyashana Senta ya vijana yenye chekechea na kozi kwa wanawake
-
TUNAWEZA, kituo kwa ajila ya vijana wagonjwa
-
UPENDO DAIMA, Senta kwa ajili ya watoto waishio barabarani
-
International Languages Training Centre iltc
-
TAHEA – Tanzania Home Economics Association
-
Radio Free Africa na Star TV
-
Bujora Cultural Centre yenye maonyesho na ngoma za kitamaduni
-
Kanisa la Nyakahoja
-
Hisani – Nyumba ya watoto
-
Hospitali ya Bugando
-
Mkutano na city director Wilson Kabwe kwenye Town Hall
Zaidi ya hayo walipata nafasi ya kufahamu Nyakato, masoko mbalimbali, na ziwa.
Wakijumlisha wageni toka Wuerzburg walikiri kwamba walitajirika sana na mambo mengi mapya waliyoyajifunza. Wakibadilishana zawadi na marafiki wa Tanzania waliagana nao na kurudi nyambani kwa safari ya masaa 30 kwa ndege.
Mwezi wa Mei 2011 watapokea Wuerzburg wanafunzi 12 pamoja na waalimu wawili toka Mwanza.