Selected Articles in Swahili languageRipoti zilizochaguliwa  kwa Kiswahili Yaliyomo ya kurasa hizi hayajamalizika bado. Tafadhali urudi hapo baadaye.

Dagaa, Ugali na Kisamvu – Wanafunzi toka Wuerzburg watembelea Mwanza

Dagaa, Ugali na Kisamvu

Kundi la wanafunzi wa domestic science toka Wuerzburg kwenye ziara ya Mwanza

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Hiki kilikuwa chakula cha kwanza ambacho Joyce Kinabo aliwatambulishia wanafunzi tisa toka Shule ya „Klara Oppenheimer“ – Wuerzburg. Kabla ya zoezi hili huyo mwalimu wa domestic science wa Senta ya VETA – Mwanza iliwaingiza wageni wake katika masharti ya kiafya (hygiene) ya Tanzania. Dagaa ni chakula kipendwacho kabisa sehemu za Lake District. Tena ugali – kila Mtanzania ugenini asifu ugali ambao ni chakula chake cha kila siku tangu siku za utoto.

Wanafunzi wawili waliwaonyesha wageni wa Kijerumani jinsi ya kula na mikono. Wajerumani walijali namna hiyo ya kula: „ni tamu zaidi ukila na mkono“.

Watanzania nao walipikiwa Kijerumani, pamoja na maonyesho ya urembo wa meza na huduma mezani. Vyakula vyote vilinunuliwa madukani na sokoni.

Waalimu Joyce Kinabo na Flaviana Minde walikuwa wamepanga ratiba kufuatana na mahitaji ya wageni. Mwalimu Doris Mehling (Wuerzburg) alitambua kwamba „kwa kweli, walijitahidi sana wakipanga ziara hiyo.“ Kufuatana na uzoefu wa Shilika la M.W.A.N.Z.A.

(Wuerzburg) wanafunzi wa Kijerumani waliweza kutembelea taasisi nyingi zaidi, kama vile:

  • Nyashana Senta ya vijana yenye chekechea na kozi kwa wanawake

  • TUNAWEZA, kituo kwa ajila ya vijana wagonjwa

  • UPENDO DAIMA, Senta kwa ajili ya watoto waishio barabarani

  • International Languages Training Centre iltc

  • TAHEA – Tanzania Home Economics Association

  • Radio Free Africa na Star TV

  • Bujora Cultural Centre yenye maonyesho na ngoma za kitamaduni

  • Kanisa la Nyakahoja

  • Hisani – Nyumba ya watoto

  • Hospitali ya Bugando

  • Mkutano na city director Wilson Kabwe kwenye Town Hall

Zaidi ya hayo walipata nafasi ya kufahamu Nyakato, masoko mbalimbali, na ziwa.

Wakijumlisha wageni toka Wuerzburg walikiri kwamba walitajirika sana na mambo mengi mapya waliyoyajifunza. Wakibadilishana zawadi na marafiki wa Tanzania waliagana nao na kurudi nyambani kwa safari ya masaa 30 kwa ndege.

Mwezi wa Mei 2011 watapokea Wuerzburg wanafunzi 12 pamoja na waalimu wawili toka Mwanza.

Hotuba ya M. Stolz – VETA-Mwanza Julai 2010

Hotuba ya Michael Stolz, VETA – Mwanza Julai 2010

Wanafunzi tisa ya Shule ya Domestic Science, Wuerzburg waliwatembelea wenzao wa VETA-Mwanza mwezi wa Julai 2010 wakiongozwa na Mwl. Michael Stolz aliye mwenyekiti wa MWANZA-Association, Wuerzburg.

Waheshimiwa mabibi na mabwana!

Awali ya yote napenda kuwashukuru sana wenyeji wetu wa VETA kwa mapokezi mazuri mliyotupatia. Napenda kumshukuru Mkuu wa Chuo, ndugu Theobald Titus Isaka. Licha ya kuwa mpya katika wajibu huu amesaidiana nasi bega kwa bega kufanikisha ziara hii. Najua kuwa ndugu Isaka ni rafiki wa udugu wetu kati ya Würzburg na Mwanza. Napenda kumshukuru Registrar Dorothy Kihampa, ambaye toka mwanzoni amesaidiana nasi kuandaa ziara yetu. Namshukuru pia mwalimu Joyce, ambaye bila shaka siku zijazo atasumbuliwa vya kutosha nasi.

Naomba sasa niutambulishe ujumbe wetu kifupi:

Huyu ni Doris Mehling, Profesa maarifa ya nyumbani. Alilipokea mara moja wazo la kutembelea Mwanza na kufanya lolote aliloweza kufanikisha safari hii. Huyu ni Homaira Mansury, Mwalimu wa Academy ya Frankenwarte. Yeye pia ametusaidia sana kufanikisha msafara wetu. Aliendesha semina ya kuwaanda wanafunzi hawa kuja huku.

Mimi mwenyewe ni Mwenyekiti wa M.W.A.N.Z.A, kikundi kilichosajiliwa rasmi na serikali yetu. Lengo letu ni kufanya udugu wa miji yetu uwe hai na udumu. Mwezi Novemba mwaka jana nilikuwa hapa pamoja na kwaya ya VOICES toka Würzburg. Tulifanikiwa kutuimbuiza mahali mbali mbali kama vile Furahisha Open Space.

Wasichana hawa wanatoka kwenye familia za kawaida kabisa na hawakuwa na fedha kugharimia safari ndefu kama hii. Ndiyo maana tulilazimika kutafuta wafadhili waliotusaidia kufanikisha ziara hii.

Tumepewa mahali pazuri sana pa kulala hapa – tunajisikia kuwa kama ujumbe rasmi wa serikali! Safari yetu ilikuwa nzuri. Wote wameguswa sana na uzuri wa mji wa Mwanza na mazingira makubwa na mazuri ya VETA.

Ukiacha mimi, wote wanatembelea kwa mara ya kwanza kabisa Afrika kusini ya Sahara. Mishangao mishangao ya mwanzoni sasa imepita na wote wanafurahia na kungojea kwa hamu mambo mengi watakayoyaona na kujifunza hapa.

Ni mara ya kwanza kabisa kwa wanafunzi wa maarifa ya nyumbani toka Würzburg kukutana na wanafunzi wenzao hapa Mwanza. Nina hakika kabisa kwamba pande zote zitajifunza mengi. Safari hii ni wanafunzi wetu watakaojifunza mengi hapa, mwakani watakuwa ni wanafunzi toka hapa watakaojifunza mengi kule Würzburg. Ni lazima tutafute wafadhili watakaosaidia gharama za safari hiyo.

Kawaida tutalazimika kuwasiliana kwa Kiingereza, lugha ambayo si rahisi kwa pande zote. Lakini nadhani tukizungumza pole pole na kutumia mikono na miguu yetu kama msaada, tutafanikiwa tu.

Nasema tena asante sana. Kama zawadi kwa VETA -Idara ya maarifa ya nyumbani na hoteli tumewaleeteni seti ya vyuma na vifaa vya jikoni, ambavyo Profesa Mehling atawakabidhi sasa.

Asante sana kwa maandalizi na mapokezi mazuri!

Ziara ya Kwaya ya VOICES

Tafrija za Kwaya „VOICES“ wakati wa ziara ya Mwanza

Jumamosi, 31.10.09

Saa 10:00 Furahisha Open Space Concert

Pamoja na Benjamin Mgonzwa na Kwaya ya MCV

 

Jumapili, 1.11.09

Ibada kwenye Kanisa la Nyakahoja

8:30 Ibada (kwa Kisuaheli)

10:15 Ibada (kwa Kiingereza)

 

Jumatatu, 2.11.09

Saa 10:00 Ktafrija Ukumbi wa Montessori

 

Jumanne, 3.11.09

Saa 10:00: Tafrija kwenye Kanisa la Sukuma