Lori la taka kabla ya kusafirishwa

Novemba 2013 M.W.A.N.Z.A. e.V. ilitoa lori la taka kwa ajili ya kusaidia usafi wa jiji la Mwanza. Lori hilo lilikuwa ni la tatu kulotewa kwa ajili ya usafi wa jiji la Mwanza, katika kipindi cha miaka 20 ya urafiki wa majiji haya mawili.

Lori lilisheheni zawadi mbali mbali, kama mavazi ya kuwakinga watu wa zimamoto, viatu kwa ajili ya watoto yatima, vifaa vya wasioona, samani mbali mbali kutoka shule za awali ya Montessori.

Lori lilifanyiwa ukaguzi uliokidhi viwango vya TÜV (car controlling) ili liweze kusaidia mji rafiki la Mwanza. Mwaka uliopita Lori hili lilikaguliwa na Tito Mahinya kutoka halmashauri ya jiji la Mwanza.

Gharama za kusafirisha lori hili hadi bandari ya Daressalam ziligharamiwa na M.W.A.N.Z.A. e.V. na wizara ya ushirikiano wa uchumi na maendeleo (BMZ, GTZ) Baada ya kufika Daressalaam serekali ya Tanzania itahusika na gharama za kutoa gari bandarini na kulisafirisha hadi Mwanza umbali wa km zisizopungua 1000.