TUNAWEZA – KITUO CHA SHUGHULI NA MSAADA WA AJIRA KWA VIJANA WENYE ULEMAVU

TUNAWEZA –
KITUO CHA SHUGHULI NA MSAADA WA AJIRA KWA VIJANA WENYE ULEMAVU

WALENGWA WETU
Tunawafundisha vijana wa dini na jinsia zote wenye ulemavu waliofikia umri wa miaka 14 na kuendelea. Kipaumbele zaidi ni vijana waliomaliza elimu ya msingi katika vitengo vya elimu maalum vilivyo katika jiji la Mwanza na maeneo ya jirani.

HUDUMA ZETU
• Tunafundisha ujuzi wa maisha na ufundi kwa kipindi cha miaka miwili
• Tunafungua kituo saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni, Jumatatu mpaka Ijumaa
• Tunawasaidia vijana kupata nafasi za kazi kulingana na uwezo na ulemavu wao
• Tunatoa ushauri kwa familia za watoto na vijana wenye ulemavu juu ya upatikanaji wa hudumu mahali tofauti
• Tunatoa semina kwa wazazi/walezi na asasi juu ya kuboresha maisha ya vijana wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na mafunzo ya lugha ya alama

KAZI ZETU ZA KILA SIKU
Vijana hujipatia maarifa ya kazi kupitia miradi tofauti.

BUSTANI
Vijana hushiriki kazi za kuanzisha na kutunza bustani za mbogamboga,
matunda na maua. Pia wanajifunza kutunza mazingira na vifaa na kutengeneza dawa kutokana na mimea ya asili.

UPISHI NA USAFI
Jikoni vijana hupika vyakula vya kiasili na vya kigeni. Wanajifunza usalama wa vyakula na matumizi sahihi ya vifaa vya jikoni.

USHONAJI NA UPIKAJI WA BATIKI
Katika miradi hii vijana wanaelekezwa jinsi ya kutumia cherehani, kutengeza batiki kwa kutumia njia tofauti na kuzalisha bidhaa rahisi ili kujiletea kipato baadaye.

ELIMU YA UJUZI WA MAISHA
Wanafunzi wetu hujifunza juu ya afya, mawasiliano na wanajamii, mambo yanayohusu thamani ya vitu na utu pamoja na utamaduni.
Zaidi ya hayo hufundishwa namna ya kuanzisha na kuendesha biashara ndogo ndogo.

USHIRIKIANO NA WAZAZI
Wazazi hukutana kila baada ya miezi miwili kujadiliana juu ya maendeleo
ya vijana wao kituoni.
Wazazi hushiriki kazi kituoni kulingana na mahitaji ili kujijengea uwezo kwa manufaa ya baadaye ya watoto wao.
Wazazi huchangia gharama kidogo kwa ajili ya chakula.

ASASI YA TUNAWEZA
Ilianzishwa na kusajiliwa mwaka 2009 na watu 12 wenye nia ya kuinua na kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu.

MALENGO YETU
• Kuwapatia vijana wenye ulemavu elimu ya ujuzi wa maisha na ufundi ili waweze
kujitegemea na kujipatia kipato
• Kuwaandaa na kuwawezesha vijana wenye ulemavu kupata na kuendelea na kazi katika soko la ajira au kujiajiri wao wenyewe baada ya kupata ujuzi
• Kuanzisha na kuendesha kituo cha kazi ambacho kinawapatia mazingira bora vijana wenye ulemavu
• Kutetea haki za watu wenye ulemavu