JIJI RAFIKI NA MWANZA LAKABIDHI MRADI KWA WAVUVI WA DAGAA ZIWA VICTORIA

Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (katikati) akibonyeza swichi ya taa za kuchaji zinazotumia umeme wa solar kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi wa uvuvi wa karabai zinazotumia nishati ya jua, kushoto kwake ni rais wa Umoja wa majiji rafiki (jiji la Wuerzburg na jiji la Mwanza) Michael Stolz’ toka nchini Ujerumani na kulia kwake ni mjumbe aliyeambatana na rais huyo, pembeni kabisa ni kiongozi wa BMU Luchelele iliyopo kata ya Mkolani ambao utakuwa ni wa majaribio kabla ya kuenea maeneo mengine kanda ya ziwa Victoria.

source www.gsengo.blogspot.com:  Saturday, November 10, 2012