Mradi mpya wa badilishiano la wanafunzi kati ya miji ya Wuerzburg na
Mwanza ulianzishwa na Frankenwarte Academy, chama cha ushirikiano kati
ya miji M.W.A.N.Z.A., na Franz-Oberthuer-shule ya ufundi. „Tutasafiri
Tanzania na kujenga mtambo wa solar tukishirikiana na wanafunzi wa
ufundi wenyeji.“ Watakaa Mwanza Oktoba 12 hadi 28.

Mwaka uliopita wanafunzi wa ufundi wa kimu toka Mwanza walizuru
Wuerzburg kwa muda wa wiki mbili. Wengi bado wanakumbuka mpambano huo
uliofaulu vizuri.

Wanafunzi watakaosafiri hivi karibuni walihudhuria semina ya maandalio
wakijiendeleza kuhusu ufahamu wa kijeografia, kihistoria, kisiasa,
kidini na kitamaduni wa Tanzania. Zaidi ya hayo walianza kujifunza
misingi ya lugha ya Kiswahili.

Licha ya mradi wa solar wanafunzi toka Wuerzburg wanatazamia kuboresha
ufahamu wao wa nchi na watu wa Tanzania. „Tutatembelea miradi ya
kijamii, taasisi za kitamaduni na pia tutashiriki katika tafrija ya Mji
wa Mwanza“. Ikiwezekana wageni hao watashiriki katika uzinduzi wa mradi
wa taa za solar wa wavuvi Luchelele ulioandaliwa na Philip Staehler.

Kwa mwaka kesho viongozi wa ushirikiano wanapanga mpambano wa wanafunzi
toka Tanzania na wenzao kwao Wuerzburg.

Maelezo ya ziada