Wanafunzi toka Mwanza watembelea Wuerzburg - Mei 2011
- Maelezo
- Jamii: Ziara kufikia Wuerzburg
Wanafunzi wa Domestic Science toka Mwanza watembelea Wuerzburg - Mei 2011
Wanafunzi wa Wuerzburg Shule ya Domestic Science, wakisaidiwa na mwalimu wao, waliandaa vifaa kama tauli vyenye majina ya wageni wao:
Wageni toka Mwanza walipokelewa na kundi toka Wuerzburg kwenye kiwanda cha ndege Frankfort.
Mwalimu Mkuu Doris Mehling (Klara-Oppenheimer-Schule), Mwalimu Homaira Mansury (Frankenwarte Akademy), Michael Stolz (Mwenyekitii wa M.W.A.N.Z.A. e.V.), Asumpta Lattus (Mtanzania, atatafsiri), na wanafunzi wanne wa domestic science waliotembelea Mwanza July 2010.
Angalia pia:
Wanafunzi toka Wuerzburg watembelea Mwanza (Mwaka wa 2010)
Mama Eva-Maria Barklind-Schwander akiwaonyesha wageni mji wa Wuerzburg awaongoza kwenda sokoni. Huyu Mama aongoza idara ya Wuerzburg International katika utawala wa mji.
TUNAWEZA - KITUO CHA SHUGHULI NA MSAADA WA AJIRA KWA VIJANA WENYE ULEMAVU
- Maelezo
- Jamii: Vyama twashirikiana navyo
TUNAWEZA -
KITUO CHA SHUGHULI NA MSAADA WA AJIRA KWA VIJANA WENYE ULEMAVU
WALENGWA WETU
Tunawafundisha vijana wa dini na jinsia zote wenye ulemavu waliofikia umri wa miaka 14 na kuendelea. Kipaumbele zaidi ni vijana waliomaliza elimu ya msingi katika vitengo vya elimu maalum vilivyo katika jiji la Mwanza na maeneo ya jirani.
HUDUMA ZETU
• Tunafundisha ujuzi wa maisha na ufundi kwa kipindi cha miaka miwili
• Tunafungua kituo saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni, Jumatatu mpaka Ijumaa
• Tunawasaidia vijana kupata nafasi za kazi kulingana na uwezo na ulemavu wao
• Tunatoa ushauri kwa familia za watoto na vijana wenye ulemavu juu ya upatikanaji wa hudumu mahali tofauti
• Tunatoa semina kwa wazazi/walezi na asasi juu ya kuboresha maisha ya vijana wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na mafunzo ya lugha ya alama
KAZI ZETU ZA KILA SIKU
Vijana hujipatia maarifa ya kazi kupitia miradi tofauti.
BUSTANI
Vijana hushiriki kazi za kuanzisha na kutunza bustani za mbogamboga,
matunda na maua. Pia wanajifunza kutunza mazingira na vifaa na kutengeneza dawa kutokana na mimea ya asili.
UPISHI NA USAFI
Jikoni vijana hupika vyakula vya kiasili na vya kigeni. Wanajifunza usalama wa vyakula na matumizi sahihi ya vifaa vya jikoni.
USHONAJI NA UPIKAJI WA BATIKI
Katika miradi hii vijana wanaelekezwa jinsi ya kutumia cherehani, kutengeza batiki kwa kutumia njia tofauti na kuzalisha bidhaa rahisi ili kujiletea kipato baadaye.
ELIMU YA UJUZI WA MAISHA
Wanafunzi wetu hujifunza juu ya afya, mawasiliano na wanajamii, mambo yanayohusu thamani ya vitu na utu pamoja na utamaduni.
Zaidi ya hayo hufundishwa namna ya kuanzisha na kuendesha biashara ndogo ndogo.
USHIRIKIANO NA WAZAZI
Wazazi hukutana kila baada ya miezi miwili kujadiliana juu ya maendeleo
ya vijana wao kituoni.
Wazazi hushiriki kazi kituoni kulingana na mahitaji ili kujijengea uwezo kwa manufaa ya baadaye ya watoto wao.
Wazazi huchangia gharama kidogo kwa ajili ya chakula.
ASASI YA TUNAWEZA
Ilianzishwa na kusajiliwa mwaka 2009 na watu 12 wenye nia ya kuinua na kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu.
MALENGO YETU
• Kuwapatia vijana wenye ulemavu elimu ya ujuzi wa maisha na ufundi ili waweze
kujitegemea na kujipatia kipato
• Kuwaandaa na kuwawezesha vijana wenye ulemavu kupata na kuendelea na kazi katika soko la ajira au kujiajiri wao wenyewe baada ya kupata ujuzi
• Kuanzisha na kuendesha kituo cha kazi ambacho kinawapatia mazingira bora vijana wenye ulemavu
• Kutetea haki za watu wenye ulemavu
Dagaa, Ugali na Kisamvu - Wanafunzi toka Wuerzburg watembelea Mwanza
- Maelezo
- Jamii: Ziara kufikia Mwanza
Dagaa, Ugali na Kisamvu
Kundi la wanafunzi wa domestic science toka Wuerzburg kwenye ziara ya Mwanza
Hiki kilikuwa chakula cha kwanza ambacho Joyce Kinabo aliwatambulishia wanafunzi tisa toka Shule ya „Klara Oppenheimer“ - Wuerzburg. Kabla ya zoezi hili huyo mwalimu wa domestic science wa Senta ya VETA – Mwanza iliwaingiza wageni wake katika masharti ya kiafya (hygiene) ya Tanzania. Dagaa ni chakula kipendwacho kabisa sehemu za Lake District. Tena ugali – kila Mtanzania ugenini asifu ugali ambao ni chakula chake cha kila siku tangu siku za utoto.
Wanafunzi wawili waliwaonyesha wageni wa Kijerumani jinsi ya kula na mikono. Wajerumani walijali namna hiyo ya kula: „ni tamu zaidi ukila na mkono“.
Watanzania nao walipikiwa Kijerumani, pamoja na maonyesho ya urembo wa meza na huduma mezani. Vyakula vyote vilinunuliwa madukani na sokoni.
Waalimu Joyce Kinabo na Flaviana Minde walikuwa wamepanga ratiba kufuatana na mahitaji ya wageni. Mwalimu Doris Mehling (Wuerzburg) alitambua kwamba „kwa kweli, walijitahidi sana wakipanga ziara hiyo.“ Kufuatana na uzoefu wa Shilika la M.W.A.N.Z.A.
(Wuerzburg) wanafunzi wa Kijerumani waliweza kutembelea taasisi nyingi zaidi, kama vile:
Nyashana Senta ya vijana yenye chekechea na kozi kwa wanawake
TUNAWEZA, kituo kwa ajila ya vijana wagonjwa
UPENDO DAIMA, Senta kwa ajili ya watoto waishio barabarani
International Languages Training Centre iltc
TAHEA – Tanzania Home Economics Association
Radio Free Africa na Star TV
Bujora Cultural Centre yenye maonyesho na ngoma za kitamaduni
Kanisa la Nyakahoja
Hisani – Nyumba ya watoto
Hospitali ya Bugando
Mkutano na city director Wilson Kabwe kwenye Town Hall
Zaidi ya hayo walipata nafasi ya kufahamu Nyakato, masoko mbalimbali, na ziwa.
Wakijumlisha wageni toka Wuerzburg walikiri kwamba walitajirika sana na mambo mengi mapya waliyoyajifunza. Wakibadilishana zawadi na marafiki wa Tanzania waliagana nao na kurudi nyambani kwa safari ya masaa 30 kwa ndege.
Mwezi wa Mei 2011 watapokea Wuerzburg wanafunzi 12 pamoja na waalimu wawili toka Mwanza.
Hotuba ya M. Stolz - VETA-Mwanza Julai 2010
- Maelezo
- Jamii: Ziara kufikia Mwanza
Hotuba ya Michael Stolz, VETA – Mwanza Julai 2010
Wanafunzi tisa ya Shule ya Domestic Science, Wuerzburg waliwatembelea wenzao wa VETA-Mwanza mwezi wa Julai 2010 wakiongozwa na Mwl. Michael Stolz aliye mwenyekiti wa MWANZA-Association, Wuerzburg.
Waheshimiwa mabibi na mabwana!
Awali ya yote napenda kuwashukuru sana wenyeji wetu wa VETA kwa mapokezi mazuri mliyotupatia. Napenda kumshukuru Mkuu wa Chuo, ndugu Theobald Titus Isaka. Licha ya kuwa mpya katika wajibu huu amesaidiana nasi bega kwa bega kufanikisha ziara hii. Najua kuwa ndugu Isaka ni rafiki wa udugu wetu kati ya Würzburg na Mwanza. Napenda kumshukuru Registrar Dorothy Kihampa, ambaye toka mwanzoni amesaidiana nasi kuandaa ziara yetu. Namshukuru pia mwalimu Joyce, ambaye bila shaka siku zijazo atasumbuliwa vya kutosha nasi.
Naomba sasa niutambulishe ujumbe wetu kifupi:
Huyu ni Doris Mehling, Profesa maarifa ya nyumbani. Alilipokea mara moja wazo la kutembelea Mwanza na kufanya lolote aliloweza kufanikisha safari hii. Huyu ni Homaira Mansury, Mwalimu wa Academy ya Frankenwarte. Yeye pia ametusaidia sana kufanikisha msafara wetu. Aliendesha semina ya kuwaanda wanafunzi hawa kuja huku.
Mimi mwenyewe ni Mwenyekiti wa M.W.A.N.Z.A, kikundi kilichosajiliwa rasmi na serikali yetu. Lengo letu ni kufanya udugu wa miji yetu uwe hai na udumu. Mwezi Novemba mwaka jana nilikuwa hapa pamoja na kwaya ya VOICES toka Würzburg. Tulifanikiwa kutuimbuiza mahali mbali mbali kama vile Furahisha Open Space.
Wasichana hawa wanatoka kwenye familia za kawaida kabisa na hawakuwa na fedha kugharimia safari ndefu kama hii. Ndiyo maana tulilazimika kutafuta wafadhili waliotusaidia kufanikisha ziara hii.
Tumepewa mahali pazuri sana pa kulala hapa – tunajisikia kuwa kama ujumbe rasmi wa serikali! Safari yetu ilikuwa nzuri. Wote wameguswa sana na uzuri wa mji wa Mwanza na mazingira makubwa na mazuri ya VETA.
Ukiacha mimi, wote wanatembelea kwa mara ya kwanza kabisa Afrika kusini ya Sahara. Mishangao mishangao ya mwanzoni sasa imepita na wote wanafurahia na kungojea kwa hamu mambo mengi watakayoyaona na kujifunza hapa.
Ni mara ya kwanza kabisa kwa wanafunzi wa maarifa ya nyumbani toka Würzburg kukutana na wanafunzi wenzao hapa Mwanza. Nina hakika kabisa kwamba pande zote zitajifunza mengi. Safari hii ni wanafunzi wetu watakaojifunza mengi hapa, mwakani watakuwa ni wanafunzi toka hapa watakaojifunza mengi kule Würzburg. Ni lazima tutafute wafadhili watakaosaidia gharama za safari hiyo.
Kawaida tutalazimika kuwasiliana kwa Kiingereza, lugha ambayo si rahisi kwa pande zote. Lakini nadhani tukizungumza pole pole na kutumia mikono na miguu yetu kama msaada, tutafanikiwa tu.
Nasema tena asante sana. Kama zawadi kwa VETA -Idara ya maarifa ya nyumbani na hoteli tumewaleeteni seti ya vyuma na vifaa vya jikoni, ambavyo Profesa Mehling atawakabidhi sasa.
Asante sana kwa maandalizi na mapokezi mazuri!
Ziara ya Kwaya ya VOICES
- Maelezo
- Jamii: Ziara kufikia Mwanza
Tafrija za Kwaya „VOICES“ wakati wa ziara ya Mwanza
Jumamosi, 31.10.09
Saa 10:00 Furahisha Open Space Concert
Pamoja na Benjamin Mgonzwa na Kwaya ya MCV
Jumapili, 1.11.09
Ibada kwenye Kanisa la Nyakahoja
8:30 Ibada (kwa Kisuaheli)
10:15 Ibada (kwa Kiingereza)
Jumatatu, 2.11.09
Saa 10:00 Ktafrija Ukumbi wa Montessori
Jumanne, 3.11.09
Saa 10:00: Tafrija kwenye Kanisa la Sukuma